19/11/2025
Tumepoteza mwanga mmoja aliyewasha vicheko kwenye nyuso za wengi. Safari ya MC Pilipili imetukumbusha kwamba maisha ni pumzi ya muda, na kila pumzi tuivutayo ni hadithi inayoweza kukoma kesho. Tuchague kuishi vizuri, kuhurumiana, kusamehe na kupenda bila kusita. Kifo hakigongi hodi, lakini hurithisha funzo: thamani ya mtu iko kwenye wema alioacha. Pumzika kwa amani Pilipili, hongera kwa alama uliyotuchorea kwenye mioyo.” 🕊️🖤