Online museum Tv show

Online museum Tv show SHINE ENTERTAINMENT it is a company deals with EVENT ORGANIZE and MANAGEMENT

 DOLA YA WACHAGGA MIAKA MICHACHE KABLA YA UHURU.Wakati wazungu wanagawana bara la Afrika, walipokuja walikuta baadhi ya ...
15/12/2019


DOLA YA WACHAGGA MIAKA MICHACHE KABLA YA UHURU.
Wakati wazungu wanagawana bara la Afrika, walipokuja walikuta baadhi ya maeneo kuna tawala zenye nguvu, zilizokua na mfumo rasmi wa uongozi. Wao waliziita tawala za jadi (Chiefdoms).

Moja ya tawala iliyokua na nguvu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ni dola ya wachagga (Chagga state). Zilikuwepo nyingine zenye nguvu k**a Himaya ya Sultani wa Zanzibar, Dola ya Buganda, Nyamwezi, Ngoni, Haya, Hutu, Tutsi, Hehe, etc.

Dola ya wachagga imetamalaki eneo la pembezoni mwa mlima Kilimanjaro kuanzia maeneo ya Rongai hadi Siha.

Eneo hili lilikua na mtawala mkuu mmoja (aliyeitwa Mangi Mkuu). Huyu alikua k**a Rais ama Mfalme wa jamii hiyo. Chini yake walikuwepo watawala wakuu wawakilishi wa majimbo. Hawa waliitwa 'Mangi Waitori'. Chini yao walikuwepo watawala wa wa maeneo madogo, hawa waliitwa Mangi k**a vile Mangi Meli wa Old Moshi, Mangi Sina wa Kibosho, Mangi Salakana wa Useri etc.

Kwa mfano eneo k**a Rombo lilikuwa na Mangi wengi. Alikuwepo Mangi wa Keni, Mangi wa Mashati, Mangi wa Mengwe etc. Lakini wote waliunganishwa na Mangi Mwitori wa Rombo. Vivyo hivyo katika maeneo ya Kibosho, Machame, Siha, Old Moshi, Marangu etc.

Mangi mdogo aliripoti kwa Mangi Mwitori. Mangi Mwitori naye aliripoti kwa Mangi Mkuu aliyeunganisha wachagga wote.

Kwa mfano kufikia mwaka 1953 Mangi Mwitori wa Vunjo alikua Petro Itosi Marealle, Mangi Mwitori wa Hai alikua Abdiel Shangali, Mangi Mwitori wa Rombo alikua James Selengia Kinabo kabla ya kustaafu mwaka 1952 na John Maruma kuchukua nafasi yake.

Mangi Mwitori alichaguliwa na wamangi wadogo. Kisha wamangi wadogo na wamangi waitori waliunda baraza kuu la uongozi (Supreme council) ambalo lilimchagua Mangi Mkuu.

January 1952 kulifanyika uchaguzi wa kumchagua Mangi Mkuu wa Wachagga. Wagombea walikua watano. Abdieli Shangali wa Machame, Jackson Kitali wa Mbokomu (Old Moshi), Petro Marealle wa Vunjo, John Maruma wa Rombo, na Thomas Marealle wa Marangu.

Baada ya kila mgombea kunadi sera zake, hatimaye kura zilipigwa na Mangi Thomas Marealle kutangazwa mshindi, akifuatiwa kwa mbali na ndugu yake Mangi Petro Itosi Marealle, aliyekuwa Mangi Mwitori wa Vunjo.

Mangi Mkuu ndiye aliyekuwa Kiongozi mkuu wa dola ya wachagga. Baraza la uongozi (Supreme council) ndicho kilikua chombo cha juu kinachosimamia utendaji wa serikali.

Kwahiyo Mangi mkuu alijitahidi sana kushirikiana mangi waitori na mangi wadogo kuhakikisha jamii nzima ya wachagga inajiletea maendeleo.

Kila Mangi alikua na baraza lake la ushauri lililojulikana k**a 'baraza la wachili', ambalo lilifanya kazi k**a baraza la mawaziri kwa sasa.

Ushirikiano huu ulifanya dola ya Wachagga kupiga hatua kubwa kimaendeleo kuliko jamii nyingi za wakati huo.

Kwa mfano kufikia mwaka 1920 dola ya wachagga ilikua ya kwanza kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kuanzisha na kumiliki gazeti lake (Komkya). Miaka 10 baadae dola ya Buganda (Buganda Kingdom) nayo ilianzisha gazeti lake (Buruuli) na mwaka 1940 Himaya ya Sultani wa Zanzibar (Zanzibar Sultanate) nayo ikaanzisha jarida lake (Imperial).

Si hivyo tu, huduma za maji, umeme, miundombinu ya barabara, hospitali na shule vilifika mapema kulinganisha na maeneo mengine ya nchi. Ikulu ya kisasa ya Mangi Mkuu wa wachagga, iliyojengwa karibu miaka 100 iliyopita ndiyo inayotumika hadi sasa k**a Ikulu ndogo ya Rais kwa mkoa wa Kilimanjaro.

Zilizokuwa ofisi za watendaji wa serikali ya Mangi mkuu (eneo la KDC Moshi) ndio ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Moshi kwa sasa.

Maendeleo haya na mengine mengi, wachagga waliamini yalitokana na elimu. Kwahiyo mwamko wa elimu ulikua mkubwa hasa baada ya wamisionari kujenga shule na huduma za afya kila walipojenga kanisa. Vitu hivi vitatu viliambatana. Kanisa, Shule, na Kituo cha afya.

Kwahiyo hata kwenye kuchagua viongozi, yule aliyekuwa na elimu nzuri ndiye aliyepewa nafasi kubwa ya kushinda ikiaminika kwamba elimu yake itachochea kasi ya maendeleo. Na hii ni moja ya sababu iliyomfanya Thomas Marealle kushinda kiti cha umangi mkuu mwaka 1952, kwani kati ya wagombea wote yeye ndiye aliyekua na shahada ya uzamili (masters degree) kwa wakati huo.

Kabla ya uhuru kulikua wachumi wawili tu wazawa ambao ni Thomas Marealle na mzee Fredrick Mchauru ambaye walisoma pamoja London School of Economics, kabla ya Marealle kupata ufadhili Cambridge University (Trinity College).

Iliaminika pia kwamba Uingereza ilitaka dola ya wachagga ijitenge kutoka Tanganyika na itafute uhuru wake yenyewe, k**a Rwanda na Burundi zilivyojitenga kutoka Tanganyika baada ya vita vya kwanza vya dunia, wakati huo zikiitwa Ruanda-Urundi.

Hata hivyo mpango huo ulishindikana kwa kuwa Tanganyika ilikua 'Trusteeship colony' ya Umoja wa mataifa, na Uingereza alikabidhiwa tu aisimamie hadi iweze kujitawala. Kwahiyo hoja ya Muingereza ilitupwa kwa maelezo kwamba wakati wa kugawanya bara la Afrika pale Berlin mwaka 1884/85 hakuna nchi inayoitwa 'Chagga state' iliyogawanywa. Hivyo uhuru unaopaswa kuwa wa Tanganyika kwa ujumla na sio wa jamii moja moja.

Baada ya jaribio hilo kushindwa, inadaiwa shirika la ujasusi la Uingereza (M16) lilimpendekeza Mangi Thomas Mareale kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika baada ya uhuru.

Katika moja ya barua za Richard Turnbull (Gavana wa mwisho wa Uingereza) kwenda kwa shirika la ujasusi la nchi hiyo (M16) ilieleza mapendekezo hayo kwa Thomas Mareale.

Sehemu ya nyaraka hiyo iliyoandikwa mwaka 1958 ilisema 'I consider Thomas Marreale an outstanding Chagga leader. I dont know him personally but he would be the leader of Tanganyika if British had to leave. However he lack support from other tribes'

Turnbull alikua akiwaelezea M16 kuhusu Mangi Thomas Marealle na umahiri wake katika uongozi. Hata hivyo alionesha hofu kuwa Marealle hakuwa na ushawishi mkubwa kwa makabila mengine nje ya wachagga.

Na hii ni moja ya hofu kubwa aliyokua nayo Mwalimu Nyerere wakati wa kudai uhuru. Alipofika uchaggani alikuta dola ya wachagga ina mamlaka kamili. Ilikua na 'well defined leadership structure', bendera yake, wimbo wake, na askari wake.

Nyerere alisema ili Tanganyika iwe uhuru lazima dola ya wachagga ife kwanza, kwa sababu hatuwezi kuwa na taifa moja ndani ya taifa jingine. Mwaka 1961 Nyerere aliagiza bendera ya Tanganyika isipandishwe kabla bendera ya wachagga haijashushwa kwanza. Tarehe 8 December 1961 saa 5 usiku bendera ya wachagga ilishushwa katika Ikulu ndogo ya Moshi, na muda mfupi baadae (saa 6 usiku, December 9) bendera ya Tanganyika ikapandishwa.

Hata hivyo hofu ya Nyerere haikua na mashiko kwa sababu Mareale mwenyewe alimpa ushirikiano mkubwa wakati wa kudai Uhuru. Na ili kuonesha kwamba hakuwa na mpango wowote wa kumhujumu, aliamua kujiuzulu nafasi yake ya umangi mkuu mwaka 1960, na kuruhusu askari wake kujiunga na jeshi la Tanganyika.

Pichani ni wagombea watatu kati ya watano walioshiriki uchaguzi wa Mangi Mkuu mwaka 1952. Kutoka kushoto ni Mangi Thomas Mareale aliyeshinda uchaguzi huo), Mangi John Maruma (Mangi Mwitori wa Rombo), na Abdieli Shangali (Mangi Mwitori wa Machame).

David Shine
Moshi.!

05/12/2019
UNAPOAMBIWA MWL.JULIUS KAMBARAGE NYERERE NI BABA WA TAIFA LA TANZANIA UWE UNAELEWA.1.Alizaliwa tarehe 13/04/1922 Butiama...
03/12/2019

UNAPOAMBIWA MWL.JULIUS KAMBARAGE NYERERE NI BABA WA TAIFA LA TANZANIA UWE UNAELEWA.

1.Alizaliwa tarehe 13/04/1922 Butiama na kufariki tarehe 14/10/1999 kule London.Ni Raisi wa kwanza Afrika kuachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe.

2.Ni Raisi wa kwanza kuhama Ikulu na kwenda kuishi kwenye nyumba aliyoijenga kwa mkopo akiwa bado Raisi.

3.Ni kati ya Raisi aliyekuwa analipwa mshahara mdogo duniani na pengine kati ya raisi aliyewahi kulipwa mshahara mdogo barani Afrika mpaka sasa.

4. Ni Mtanganyika wa kwanza kusoma chuo kikuu nchini Uingereza na Muafrika wa pili kupata Degree nje ya Afrika, akisomea English, Political Economy, Social Anthropology, British History, Economic History, Constitutional Law, and Moral Philosophy.

5. Ni kiongozi aliyeisaidia China kuingia Umoja wa Mataifa na hotuba yake maarufu akisema
kwamba,"Umoja wa Mataifa si serikali ya dunia bali ni sehemu ambayo dunia nzima inakutana,
kwahiyo kumtoa China katika umoja wa mataifa ni kumtoa kuwa sehemu ya dunia".

6. Ndio mwanzilishi wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini- Anti Apartheid Movement mwaka 1959 pamoja na Trevor Huddleston nchini Uingereza.

7. Ni mmoja kati ya waanzilishi wa Umoja wa Afrika, 1963.

8. Amezisaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru kuliko mtu mwingine yoyote katika historia ya ukoloni, nchi hizo ni Zambia (1964), Malawi (1964), Botswana (1966), Lesotho (1966), Mauritius (1968), Swaziland (1968) and Seychelles (1976) na baadae 1975 (Mozambique), (Angola), 1980 (Zimbabwe), 1990
(Namibia) na 1994 (South Africa).

9. Mwaka 2009 alitajwa na raisi wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa k**a "World Hero of Social Justice".

10. Amepokea shahada mbalimbali kutoka, University of Edinburgh (UK), Duquesne University (USA), University of Cairo (Egypt), University of Nigeria (Nigeria), University of Ibadan (Nigeria), University of Liberia (Liberia), University of Toronto (Canada), Howard University (USA), Jawaharlal Nehru University (India), University of Havana (Cuba), National University of Lesotho, University of the Philippines, Fort Hare University (South Africa),Sokoine University of Agriculture (Tanzania), and Lincoln University (PA, USA).

11. Alipokea Tuzo ya Order of José Marti Cuba 1975, Order of the Aztec Eagle (Collar) Mexico 1975, Order of Amílcar Cabral Guinea Bissau 1976, the Nehru Award for International Understanding in 1976, the Third World Prize in 1982, Order of Eduardo Mondlane
Mozambique 1983, the Nansen Medal for outstanding services to Refugees in 1983, Order of Agostinho Neto Angola 1985, Sir Seretse Khama SADC Medal 1986, Joliot-Curie Medal of Peace 1988, the Lenin Peace Prize in 1987, the International Simón Bolívar Prize in
1992, and the Gandhi Peace Prize in 1995, Statesman of the 20th century by the Chama Cha Mapinduzi 2000, Order of the Companions of O. R. Tambo (Gold) South Africa 2004, Royal Order of Munhumutapa Zimbabwe 2005, Most Excellent Order of the Pearl of Africa (Grand Master) Uganda 2005, Order of Katonga Uganda 2005, National Liberation Medal Rwanda 2009, National Liberation Medal Rwanda 2009, Campaign Against Genocide Medal Rwanda 2009, Order of the Most Ancient Welwitschi Mirabilis Namibia 2010, Tanzania Professional Network Award 2011, Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Tanzania 2011, National Order of the Republic (Grand Cordon) Burundi 2012 and Order of Jamaica, Jamaica.

12. Mwaka 2007 Rais Yoweri Museveni wa Uganda alimpa tuzo ya Katongo, Medali ya juu kuliko zote ya Jeshi la Uganda kwa heshima ya upinzani wake dhidi ya ukoloni na serikali ya Idi Amin.

13. Mitaa, barabara, majengo, vituo, shule, vyuo na vitu vilivyopewa jina lake; Daraja la Nyerere Kigamboni,Julius Nyerere University of Kankan, in Kankan, Guinea, Nyerere Drive,Gaborone (1.6 km) in Botswana, Nyerere Avenue, Mombasa (1.5 km)
and Nyerere Road, Kisumu (2 km) in Kenya, Julius Nyerere Street, Windhoek (1.1 km) in Namibia, Julius Nyerere Street, Durban (0.5 km) in South Africa, Nyerere Road, Kitwe (1.4 km) in Zambia, Julius Nyerere Way, Harare (1 km) in Zimbabwe, Julius Nyerere International Airport, Julius Nyerere International Convention Centre, Nyerere Day- Public Holiday 14/10, Nyerere Cup, Nyerere Road, Unguja, Zanzibar (6.5 km), Nyerere Secondary School in Mwanga District and J.K. Nyerere Secondary School in Moshi, Kilimanjaro Region, Mwalimu J. K. Nyerere Secondary School in Mbozi District, Mbeya Region, Nyerere Memorial School in Korogwe, Tanga Region, Nyerere High School Migoli in Iringa Region, Nyerere Secondary School in Unguja, Zanzibar, Mwalimu Nyerere Foundation, Mwalimu Nyerere Museum Centre and Mwalimu Nyerere Memorial Academy- Tanzania.

14. Baadhi ya vitabu alivyoviandika ni, Freedom and Unity (Uhuru na Umoja), Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa), The Arusha
Declaration, Education for self-reliance, The varied paths to socialism, The purpose is man, Socialism and development, Freedom and Development (Uhuru Na Maendeleo), Ujamaa, Crusade for Liberation, Education for Self-Reliance, na Uongozi na Hatima ya Tanzania.

15. Pamoja na kujulikana k**a - Baba wa Taifa la Tanzania, Nchi za Kusini mwa Afrika zinamtambua k**a baba wa Ukombozi wa Nchi za Kusini.

16. Pamoja na kujua lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa Ufasaha - pia alikuwa akifahamu lugha ya Kigiriki na Kilatini.

17. Julius Nyerere ameandikwa kwenye kitabu cha Enyclopia k**a mtu pekee duniani katika historia ya karne ya 21, aliyeweza kuwafanya watu wa makabila, dini, asili na historia tofauti kujiona k**a watu wamoja.

SHARE

http://PartTimeJob.online/?user=680001
08/09/2018

http://PartTimeJob.online/?user=680001

PartTimeJob.online - We has been around since years and has over thousands members worldwide. There are no fees to join, and we send out thousands of dollars in payments to our members every month.

Audio :Rayvanny - Jikatae: Download MP3
22/02/2018

Audio :Rayvanny - Jikatae: Download MP3

Tanzania Number One Website that give you all trending Entertainment News, New Audio and New Video, New Movies, New and Many more

Audio :Diamond Platnumz FT.Yvonne Chaka chaka Eddy Kenzo Kcee Vanessa Mdee: Download MP3
22/02/2018

Audio :Diamond Platnumz FT.Yvonne Chaka chaka Eddy Kenzo Kcee Vanessa Mdee: Download MP3

Tanzania Number One Website that give you all trending Entertainment News, New Audio and New Video, New Movies, New and Many more

Audio :Bill Nass Ft Barnaba - Demu Gani: Download MP3
21/02/2018

Audio :Bill Nass Ft Barnaba - Demu Gani: Download MP3

Tanzania Number One Website that give you all trending Entertainment News, New Audio and New Video, New Movies, New and Many more

Audio :Barnaba - ushawahi: Download MP3
21/02/2018

Audio :Barnaba - ushawahi: Download MP3

Tanzania Number One Website that give you all trending Entertainment News, New Audio and New Video, New Movies, New and Many more

Audio :Barnaba - milele daima: Download MP3
21/02/2018

Audio :Barnaba - milele daima: Download MP3

Tanzania Number One Website that give you all trending Entertainment News, New Audio and New Video, New Movies, New and Many more

Audio :Barnaba ft p**i njia panda: Download MP3
21/02/2018

Audio :Barnaba ft p**i njia panda: Download MP3

Tanzania Number One Website that give you all trending Entertainment News, New Audio and New Video, New Movies, New and Many more

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00

Telephone

+255719971313

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Online museum Tv show posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Online museum Tv show:

Share

Category