06/16/2026
Leo naomba kuongea na SIMBA..!π¦ kidogo
Bro Mimi hua najiuliza mengi saana kuhusu matendo ambayo hua unafanyia wasanii wenzio sio Poa ni kweli wewe ni biggest artist kwa east Africa but watakao kuja kukuangusha ni hao machawa wako
Hivi ni kwanini kila msanii alietoka WCB lazima uwe na bifu nae?
1. Alipo ondoka Billionea kid π° WCB aliundiwa zengwe la kufa mtu na kusambaza chuki kwa watu ili waweze kumchukia mtoto wa mama Richard ambapo ulifanikiwa coz mpaka leo kuna media ambayo haiwezi piga ngoma za rich kisa tu vijisenti vya kunywa maji
2. Kaondoka KONDEBOY WCB nae aliundiwa zengwe laajabu mpaka hata Mimi mliwai kunitumia niweze kumu attack kwakunipa evidence za uongo zidi yake wakati haikua kweli na mpaka leo hua unatamani apotee kimziki je! Hua unataka ubaki kua artist pekeako?
3. Kaondoka Rayvanny Artist pekee mwenye BET AWARD Tanzania nzima nae kwa sasa ushamkunjia kisa tu maneno ya kuletewa mezani bila kuchunguza, but huyu huyu ndo kaiwakilisha Tanzania kwenye FIFA WORLD CUP COUNTDOWN CEREMONY nilitegemea ungekua wa kwanza kumpongeza na kua proud nae Ila ndo kwanza limekuongezea chuki kwenye moyo wako
4. Mbosso the same now umemgieuza kua adui wako mkubwa pasipo sababu, kipindi mbosso anajipanga kuachia EP ROOM NUMBER 3 mbosso alitangaza tareh then na wewe tareh ilipofika mapema tu ukaharibu kwakuachia WIMBO wako na bien WIMBO ambao uli trend kwa siku3 ukapotea, but mbosso alipoachia EP yake WIMBO wa PAWA ukaruka kitu ambacho kimekuuma mpaka leo
Sasa swali langu kwako ni kwanini kila artist anae toka WCB hua unamgieuza kua Adui wako mkubwa ?
Mbona wewe ulipoondokaga Sharobaro record Bob Junior hakuwai kukutoza hata senti 1 ao kukugieuza kua Adui wake number one, Why always you?
Alafu Kingine hiii dunia ni tambara bovu k**a ni umaarufu wewe bado saana k**a ulikua hujui Tanzania mpaka leo hakuna artist yeyote ambae kashafikia record ya Mrnice TZ enzi zake alikua anapiga show kwenye stadium only na alikua ana piga soldout zoote
Jamaa nyimbo zake zili hit dunia nzima na ikumbukwe enzi hizo kulikua hakuna instagram wala Tiktok wala WhatsApp haikuwepo hata flash disc hazikuwepo Ila jamaa alikua na pesa balaa but leo je? Be humble ..