04/06/2025
Zimebaki siku Saba kuelekea Tamasha la Uwekezaji Zanzibar 2025 (ZIS) ambalo linatarajia kufanyika katika maeneo huru ya Uwekezaji Micheweni Pemba Juni 12 hadi 15, 2025.
Tamasha hili kubwa linakusudia kuonesha fursa mbalimbali na halisi za Uwekezaji zinazopatikana visiwani Zanzibar, hususan katika sekta ya Utalii, Uchumi wa Buluu, Kilimo na Biashara ya mazao, Nishati mbadala, ICT na Ubunifu, Maendeleo ya miundombinu, Elimu na huduma za Afya.
Tamasha hili litajumuisha, Maonesho ya kibiashara, Matembezi ya hiari, Warsha na mijadala mbalimbali ya kibiashara, Ziara za miradi ya Uwekezaji, Mkutano wa Wafanya Biashara (B2B) na Chakula cha Jioni (Gala Dinner) pamoja na Kambi ya Matibabu.
Washiriki wa Tamasha hili, Taasisi za Umma na Binafasi,Wawekezaji, Wafanyabiashara Wakubwa wa Kati na Wadogo, Viongozi wakuu wa kitaifa na kimataifa, Wanasiasa, Viongozi wa Dini na wananchi kwa ujumla.
Kaulimbiu yetu ikiwa ni “Ni muda wa Pemba sasa”, mwaka huu kongamano limeelekezwa katika kuhamasisha Uwekezaji wa kimkakati kisiwani Pemba mahali penye fursa, uzuri wa asili, na utulivu.
KARIBUNI SANA
’sTimeForPemba!