30/03/2025
MZIGO WA MAHABA – SEHEMU YA PILI
📝Ray Shayo
☎️0678236344
Amani alijikuta akitazama simu yake kwa muda mrefu, akipitia ujumbe wa mwisho aliotumiwa na Neema. Ilikuwa ni ujumbe mfupi lakini wenye uzito :
"Amani, kuna jambo nataka kukuambia... lakini siwezi kwa meseji. Naomba tuonane."
Moyo wake ulishtuka kidogo. Neema hakuwa mtu wa maneno mengi, na kila aliposema kuna jambo la muhimu, basi hakika lilikuwa na uzito.
"Labda ni kuhusu Faraji…" alijiwazia. Kwa muda mrefu, Amani alikuwa akihisi kuna kitu hakiko sawa kati ya Neema na Faraji, lakini hakujua ni nini hasa.
Alikata shauri, akampigia Neema. Simu iliita mara mbili kabla haijapokelewa.
"Haloo, Neema…" sauti yake ilikuwa ya upole.
"Haloo Amani, umeiona meseji yangu?" Neema aliuliza kwa sauti ya wasiwasi.
"Ndio, na ndio maana nakupigia. Tunaweza kuonana lini?"
"Kesho jioni, sehemu ile ile."
Amani alijua sehemu anayomaanisha – duka la kahawa walilopenda kukutana, mahali ambapo mara nyingi walikaa na kuzungumza kuhusu maisha yao.
Usiku huo, Amani alijikuta akihangaika kitandani. Fikra zake zikiwa na maswali lukuki.
"Neema anataka kuniambia nini?
Labda ni kuhusu Faraji? Au kuna jambo jingine kubwa zaidi?" Amani aliwaza pasipo kuwa na jibu
Kesho yake jioni, alipofika kwenye duka la kahawa, alimkuta Neema akiwa tayari ameketi kwenye kona ya dirisha, akizungusha kijiko kwenye kikombe chake cha kahawa huku akionekana mwenye mawazo mazito.
Amani alipoketi, Neema alimtazama kwa macho yaliyojaa hisia…
"Amani, kuna jambo lazima nikwambie, lakini naogopa litabadilisha kila kitu kati yetu…"
Je, 🤷Neema ana siri gani? Sehemu ya tatu itafichua mambo mazito! Usikose