11/06/2022
Papa Francisko analazimika kuhairisha tarehe zilizokuwa zimepangwa za ziara yake ya Kitume barani Afrika, katika Juma la kwanza la Mwezi Julai ambalo lingemwona huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Sudan Kusini.
Ni taarifa iliyotolewa asubuhi, tarehe 10 Juni 2022 katika Ofisi za Vyombo vya habari Vatican na Msemaji wake Dk Matteo Bruni.
“Kwa kupokea ushauri kutoka kwa Madaktari, ili kutobatilisha matokeo ya matibabu ya goti ambayo bado yanaendelea, Baba Mtakatifu Francisko kwa masikitiko amelazimika kuhairisha Ziara yake ya Kitume katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini, iliyokuwa inatazamiwa mnamo tarehe 2 hadi 7 Julai na tarehe nyingine itaandaliwa.”
"Mhujaji barani Afrika alitazamiwa kwenda sehemu mbili, nchini Congo katika mji Mkuu wa Kinshasa na katika mji wa Goma na wakati huo huko huko Sudan Kusini, katika Mji Mkuu Juba".
Hata hivyo "kuhairisha ziara hiyo sio kuifuta", amefafanua hivyo Msemaji wa vyombo vya habari Vatican, Dk. Matteo Brun wakati akijibu maswali kwa waandishi wa habari na kwamba "kumekuwapo na matokeo mazuri katika kufanya mazoezi, hivyo madaktari wamemshauri Papa asilazimishe sana mguu wake ambapo unaweza kurudisha nyuma hali na kupoteza unafuu alioanza kuwa nao".....
|||||
ZAMUYANGU
#