19/09/2026
Kocha wa Club Fit, Salim Rajab Amani, amesema amefurahishwa na timu yake kufuzu hatua ya 16 bora ya Rashidabdallah_supercup (RASC) 7th Edition, akieleza kuwa ushiriki wao kwenye mashindano hayo umewapa wachezaji nafasi muhimu ya kupata uzoefu na kuonyesha vipaji vyao.
“Nasikia fiti. Ni mara yetu ya kwanza kushiriki kwenye the biggest tournament in Kenya, RASC. Ni experience kubwa kwa wachezaji wangu. Wamekuja kujibamba, kushowcase talent zao, na kwa bahati nzuri tumepata ushindi kupitia penalties na kufuzu Round of 16.”
Amani amesema nidhamu, umakini na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi vilikuwa muhimu katika kupata ushindi huo.
“Dedication ya players, focus yao pamoja na kufuata maagizo ndiyo imetusaidia. Tulianza game tukiwa top, halafu tukasawazishwa, lakini tukapush hadi penalties. Alhamdulillah, tukapata ushindi.”
Akizungumzia wapinzani wao, Amani amesema Club Fit ilipata changamoto kubwa katika kipindi cha kwanza kutokana na pressing ya juu ya Dzitsulu FC.
“First half ametukujia vizuri, amekuwa na high press na hatukuwa tumejipanga. Ametuumiza kichwa k**a technical bench. Tukaenda half time, tukajipanga upya. Mpinzani wangu amekuwa good opponent na tumejifunza vitu vingi. Ukiangalia squad yake, inaonekana wana vijana wengi wadogo, lakini wametupa competition kubwa. Kwa hiyo, tumejifunza mengi.”
Kuhusu mipango yao kuelekea hatua ya 16 bora, kocha huyo amesema wataanza kwa kumchambua mpinzani wao kabla ya kurejea uwanjani kurekebisha mapungufu yaliyoonekana katika mchezo huo.
“Kwanza tutakuja kuona game ya our next opponent, tuone vile wanacheza. Then tutaenda drawing board kurekebisha makosa machache tuliyofanya leo. Ninaamini kwenye game inayofuata tutakuja kuonyesha kitu kizuri kwa fans.”
Rashid Abdalla Lulu Hassan Rasi Mangale Suleiman Bamsuley Abdallah Marere Mwakulinga